Thursday, February 12, 2009

MPIJI-MAGOHE NA CHANGAMOTO TISA


Shule ya sekondari ya Mpji-magohe ni miongoni mwa shule za Serikali za kata ililyoanzishwa mwaka 2006 na hadi hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 829 kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne, ambapo wasichana ni 410 na wavulana ni 410.

Mpji magohe ni shule iliyopo umbali wa 10 km kutoka katika barabara kuu ya Morogoro jijini Dar es salaam

Shule hii mbali na kufanya vizuri kiasi katika elimu imekuwa ikikabiliwa na matatizo chungu mzima kama vile kukosekana kwa usafiri wa uhakika toka mbezi hadi mpiji kwa kuwa wanafunzi wengi makazi yao ni katika mji mdogo wa Mbezi jijini hapa.

Miongoni mwa kero zinazosababisha kutolewa kwa elimu chini ya kiwango ni pamoja na kuwepo kwa uhaba wa walimu wa sayansi na Hisabati, Uhaba wa vitabu vya kufundishia na maktaba, kukosekana kwa maabara ya utekelezaji wa masomo kwa njia ya vitendo.

Mkuu wa shule hiyo Bagaya Kashato anasema mbali na changamoto hizo pia kukosekana kwa maji na umeme pia kunachangia kwa njia moja au nyingine kupoteza muelekeo wa jitihada za wanafunzi katika kuhakikisha kuwa wanafanya vizurio katika mitihani yao.

Anasema nyumba za walimu nazo pia zimetoa mwanya wa kwa wanafunzi kindwa madarasani, ukiachilia mbali uhaba wa thamani kwa waalimu na wanafunzi.

Anasema edapo Serikali ikifanya jitihada za kuhakikisha inaondoa sehemu ya kero huizo katika shule za kati basi elimu itakayo kuwa inatolewa itazingatia vigezo vyote vya kitaaluma.

By Prince P

No comments:

Post a Comment