Tuesday, February 10, 2009

RAIS KIKWETE HAPO BRAVO

Ni vema na haki kusifu ama kupongeza jambo zuri linapofanywa na viongozi wetu wa serikali kijamii, kisiasa na hata kitamaduni.

Mambo haya hakika mbali na kuhamasisha jamii yanaleta uamsho ama morari wa kuongeza nguvu katika jambo fulani.

Mapema siku ya jana Rais Jakaya Kikwete aliweza kuongea na wachezaji wa timu ya Taifa Stars katika eneo la ikulu na kisha kuwatia moyo katika safari yao ya fainali za kombe la CHAN linalowahusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Akizungumza nao aliwaeleza nini wanachotakiwa kukufanya kwa timu hiyo akidai “Watanzania tunataka raha, tupeni raha jamani” alisisitiza kikwete, huku akipokewa na sauti zilizosikika kuwa hatutakuangusha tutapigana kufa na kupona kulinda heshima ya taifa

Mfano huu wa rais Kikwete hakika ni wa kuigwa kwa asilimia kubwa kwani viongozi wengibne wakifanya jambo hili maendeleo katika jamii yanaweza kuonekana kwa kasi kubwa hapa nchini.
Peter.

No comments:

Post a Comment