Katika hali ya kusikitisha imeonyesha kuwa kiwango cha kufaulu kikishuka kwa wastani wa asilimia sita nukta moja ikilinganishwa na mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mtendaji wa baraza hilo DK Joyce Ndalichako, watahiniwa 29,239 sawa na asilimia 87.21 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu mwaka huu ambapo waliofaulu mtihani huo mwaka jana walikuwa sawa na asilimia 93.31 ya watahiniwa.
Sekondari ya wasichana ya Kifungilo imeongoza katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 25, ikifuatiwa na shule ya wasichana ya Mpanda, Seminari ya Mtakatifu James, sekondari ya Changarawe na sekondari ya Nyerere - Migori wakati shule zilizofanya vibaya katika kundi hilo ni Lake, Ifunda - wasichana, Maswa, Zanzibar Commercial, Lumumba, Hamamnii na ufundi Ifunda.
Nadhani kuna kila haja kwa Wizara husika ikishirikiana na wataalamu wake kuhakikisha kuwa inapambanua chanzo kilicho sibu wanafunzi mwaka huu kushuka kiwango cha ufaulu badala yan kuendelea kupanda.
Lakini ninachoweza kushauri ni kwamba elimu nchini haitaweza kubadilika kama walimu wakiendelea kudharauliwa na kupewa ujira mdogo ambao unawashawishi kubuni mambo yao mengine ya kuweza kuwaingizia kipato na kuacha kabisa kuzingatia kuhusu taaluma yao ya kufundisha.
No comments:
Post a Comment