Miezi mingi iliyopita niliwahi kusikia Mbunge mmoja akiongea kwenye mkutano wa bunge kuwa watanzania wote ni mafisadi,kauli hiyo ilimkosesha raha Spika Sitta na kumtaka mbunge huyo aliombe radhi bunge kwani akisema watanzania wote ni wezi basi hata rais pamoja na waheshimiwa wabunge ni wezi pia.
Lakini ukweli mni upi basi,hivi karibuni tumesikia minong'ono mikubwa inayomhusu mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi pamoja na mbunge Rostam Azizi.
Mengi anadai kuwa Rostamu ni Fisadi Papa, akimaanisha kuwa amekubuhu katika kufisadi mali za umma ikiwa ni pamoja na kujilimbikizia mali isivyo halali.
lakini naye Rostam akukaa kimya ameibuka na kudai kuwa Mengi ni nyangumi wa ufisadi, hivi ni vichekesho sana nadhani hawa mabwana wote wawili hawana maana ila wote wanapiga kelele kwa maana ya kutajka kujisafisha maovu yao.
Kinachofanyika hapa ni kila mmoja anatafuta nguvu ya kijamii, nadhani muda wenu ungalipo bado kitambo kidogo tu maovu yenu yatakuwa peupe,Ingelikuwa vyema mkakimbilia Yordan mkaoge ili mtakasike na kuwekwa huru na laana hii ya ufisadi.
Ninacho jua mimi mlevi hawezi kumtukana mtu safi ila mtu humtukana mlevi mwenzake, kadhalika fisadi hawezi kurushiana maneno na mtu asiye nacho bali fisadi kwa fisadi ukiwaweka pamoja watagombana tu, Mbona mnasahau elimu ya sumaku always negative na positive zinashabihiana lakini Positive kwa positive du!!,
No comments:
Post a Comment