Monday, March 16, 2009

Rais Kikwete tunasubiri asali ya London


Mapema siku ya jana Rais Jakaya kikwete aliondoka nchini yeye na wajumbe kadhaa kwa lengo la kuhudhuria mkutano mkubwa wa G-20 utakaofanyika nchini Uingereza katika jiji la London.

Wapo watu wengi wanaohoji kuhusu umuhimu wa safari hizo za rais kama ni bora na zinamanufaa kwa uchumi wa taifa hili changa.Pengine wamesahau uule usemi unaosema ndondondo si chururu

Katika hali hii wasomi na wadau mbalimbali wamediliki hata kueleza kuwa ni vema rais akapunguziwa ziara za kutoka nje kwani zinakuwa zikitumia mabilioni ya fedha ambazo zingetumika katika kutafuta pembejeo za kilimo na kununua madawa ya hospitalini.

Huu ni ukweli kabisa kwamba safari hizi zinapunguza kwa kiasi fulani pato la taifa kwa kuoneza matumizi,lakini cha kujiuliza ni je Taifa h ili linauwezo wa kusimama kwa miguu yake bila kupata misaada kutoka kwa wahisani.

Lakini pia fedha za kilimo na mambo mengi zinatokana na wahisani, je ni nani aliyezishughulikia au zilishuka kama mana jangwani.ya ‘Mungu mengi’ huu ni unafiki mkubwa wa baadhi ya viongozi na wasomi wanosema kuwa safari hizo hazina ulazima wowote

Tumeshughudia ziara nyingi anazofanya raisi katika nchi mbalimbali zikileta mafanikio kwa Tanzanuia, mambo haya ni pamoja na kufutiwa madeni na kupewa mikopo nafuu ambayo hadi hivi leo imekuwa suluhisho la baadhi ya kero za wananchi.

Mimi ninaamini kabisa kuwa Rais Kikwete ni mwadilifu na mchapakazi hodari hivyo anapoamua kulivalia njuga suala fulani hulitizama kwa pande zote , yaani kwa kuangalia faida na hasara zake.

Hivyo ni vema rais akaendelea kufanya safari zake nje ya nchi kwa kwenda mbele kwani watanzania tunaona matunda yake kila kunaopoitwa leo.

Amby.