Wednesday, May 27, 2009

CCM poll victory confirms party’s hold on rural electorate



By Prince Pierre

Civic United Front (CUF) leader Prof Ibrahim Lipumba has argued that existing constitution and lack of voter education has played a role in the opposition’s defeat in recent polls in Busanda.

CCM has maintained its winning trend after defeating three opposition parties including Chadema an immediate opponent by a significant margin. The campaign was mainly marked by fierce rivalry between CCM and Chadema.

According to the party’s Publicity Secretary Capt. John Chiligati. CCM candidate’s victory is attributable to party’s rigorous move to implement its manifesto, a trend that transforms the lives of the poor.

However, scores of analysts who were reached for comments said that voters in rural areas could easily give in due to threats and ignorance over lack of civic education, although to a certain extent people might still be trusting CCM.

Announcing to the final results by Busanda Returning Officer Mr Dan Mollel, the winner was CCM’s candidates Ms. Leonsia Bukwimba who garnered 29,242 votes against her immediate opponent Chadema’s Mr Finias Magessa who scooped 22,799 votes.

Other candidates with the names of their parties in brackets are Mr Oscar Ndalawa (CUF) and Mrs. Beatrice Lubambe (UDP) scooped 957 and 271 votes respectively.

Tuesday, May 5, 2009

NYANGUMI NA PAPA WOTE WEZI, 'PUMBAVU ZENU'


Miezi mingi iliyopita niliwahi kusikia Mbunge mmoja akiongea kwenye mkutano wa bunge kuwa watanzania wote ni mafisadi,kauli hiyo ilimkosesha raha Spika Sitta na kumtaka mbunge huyo aliombe radhi bunge kwani akisema watanzania wote ni wezi basi hata rais pamoja na waheshimiwa wabunge ni wezi pia.


Lakini ukweli mni upi basi,hivi karibuni tumesikia minong'ono mikubwa inayomhusu mfanyabiashara maarufu nchini Reginald Mengi pamoja na mbunge Rostam Azizi.
Mengi anadai kuwa Rostamu ni Fisadi Papa, akimaanisha kuwa amekubuhu katika kufisadi mali za umma ikiwa ni pamoja na kujilimbikizia mali isivyo halali.
lakini naye Rostam akukaa kimya ameibuka na kudai kuwa Mengi ni nyangumi wa ufisadi, hivi ni vichekesho sana nadhani hawa mabwana wote wawili hawana maana ila wote wanapiga kelele kwa maana ya kutajka kujisafisha maovu yao.
Kinachofanyika hapa ni kila mmoja anatafuta nguvu ya kijamii, nadhani muda wenu ungalipo bado kitambo kidogo tu maovu yenu yatakuwa peupe,Ingelikuwa vyema mkakimbilia Yordan mkaoge ili mtakasike na kuwekwa huru na laana hii ya ufisadi.
Ninacho jua mimi mlevi hawezi kumtukana mtu safi ila mtu humtukana mlevi mwenzake, kadhalika fisadi hawezi kurushiana maneno na mtu asiye nacho bali fisadi kwa fisadi ukiwaweka pamoja watagombana tu, Mbona mnasahau elimu ya sumaku always negative na positive zinashabihiana lakini Positive kwa positive du!!,

Hongereni form 'Six', BIla kuboresha mazingira ya walimu haiwezekani

Mapema wiki iliyopita matokeo ya kidato cha sita yaliweza kutangazwa na na Baraza la mitihani la Tanzania - NECTA sambamba na hilo pia baraza hilo lilitangaza matokeo ya stashahada ya ualimu iliyofanyika mwezi wa pili, mwaka huu

Katika hali ya kusikitisha imeonyesha kuwa kiwango cha kufaulu kikishuka kwa wastani wa asilimia sita nukta moja ikilinganishwa na mwaka jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mtendaji wa baraza hilo DK Joyce Ndalichako, watahiniwa 29,239 sawa na asilimia 87.21 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu mwaka huu ambapo waliofaulu mtihani huo mwaka jana walikuwa sawa na asilimia 93.31 ya watahiniwa.

Sekondari ya wasichana ya Kifungilo imeongoza katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 25, ikifuatiwa na shule ya wasichana ya Mpanda, Seminari ya Mtakatifu James, sekondari ya Changarawe na sekondari ya Nyerere - Migori wakati shule zilizofanya vibaya katika kundi hilo ni Lake, Ifunda - wasichana, Maswa, Zanzibar Commercial, Lumumba, Hamamnii na ufundi Ifunda.
Nadhani kuna kila haja kwa Wizara husika ikishirikiana na wataalamu wake kuhakikisha kuwa inapambanua chanzo kilicho sibu wanafunzi mwaka huu kushuka kiwango cha ufaulu badala yan kuendelea kupanda.
Lakini ninachoweza kushauri ni kwamba elimu nchini haitaweza kubadilika kama walimu wakiendelea kudharauliwa na kupewa ujira mdogo ambao unawashawishi kubuni mambo yao mengine ya kuweza kuwaingizia kipato na kuacha kabisa kuzingatia kuhusu taaluma yao ya kufundisha.

Friday, May 1, 2009

Jiji la Dar es Salam matatani


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia athari za mabomu yaliyotokea katika kambi ya jeshi eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam.