Saturday, February 7, 2009

Kilichotokea Dodoma ni kizungumkuti


Mapema juzi tumeuhudia jambo ambalo baadhi ya vyombo vya habari vimeweza kuliripoti kinagaubaga nikiwa namaanisha ku waandishi waliweza kulitukuza na kuliandika kuwa Dk Slaa atumiwa majasusi, wengine ategewa vinasa sauti, wengine wakieleza kuwa amepangiwa njama za kumuangamiza kabisa kisiasa.

Hiki ni kitendawili kwa kweli, jambo hili ni wizi mtupu, kwani ukijaribu kwenda mbele na kurudi nyuma utagundua kuwa mambo mengi yasiyokuwa na msingi huwa yanatokea katika kipindi cha bunge hasa mahali ambapo mada ngumu zinapokuwa zikihadiliwa.
Nasema huu ni wizi mtupu ni vema wahusika wakagundua kuwa njama hizo za kulipua mambo ili tu kuwapoteza malengo wananchi ambao wanafuatilia kwa umakini shughuli za bunge zimepitwa na wakati, badala yake wanatakiwa kfikiri mbinu zingine za kuwapoteza maboya wananchi.

Mimi nataka kufahamu, kuna mambo mengi mazuri yaliyokuwa yakiendelea bungeni lakini kutokana na kutokea kwa jambo hilo vyombo vya habari vilisahau kuyapa kipaombele mambo ambayo kwa namna moja au nyingine ni sehemu ya kuondokana kwa umaskini kwa mtanzania wa hali ya chini kabisa.

“huu ni wizi,tena wizi mtupu ni vema watu wakafungua macho na kuangalia mbele ili waone” ushauri wangu kwa watanzania ni kuhakikisha kuwa jambo hilo la Slaa na mwenzake halipewi kipaombele bali warudi nyuma na kuyaangalia mambo yao waliyokuwa wakiyafuatilia bungeni.

Mguso

No comments:

Post a Comment